Tuesday, 16December, 2025    7:07 pm

Play Listen Live

Visa vya ulawiti vimeongezeka kaunti ya Kwale, mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameingilia kati.

Mashirika ya kijamii yakiongozwa na shirika la Samba Sports Youth Trust yameelezea hofu kufuatia ongezeko la visa vya ulawiti katika kaunti ya Kwale.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Kinondo Mkurugenzi wa shirika hilo Mohammed Mwachausa amesema hali hiyo inachangia ukiukaji mkubwa wa haki za watoto.

Kwa upande wake afisa wa tume ya kutetea haki za kibinadamu nchini KHRC Irene Soila ameitaka serikali kuangazia kwa kina suala hilo akisema tume hiyo inashirikiana na mashirika ya kijamii kaunti ya ya Kwale ili kutafuta suluhu la tatizo hilo.

 

Story by Janet Shume

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.