Monday, 19January, 2026    9:30 am

Play Listen Live

Mkuu wa majeshi Jenerali Charles Kahariri amefanya ziara yake katika kambi ya kijeshi ya Manda Bay, Lamu

Mkuu wa majeshi nchini jenerali Charles Kahariri ametoa hakikisho kwamba idara ya ulinzi KDF imejikitika kuhakikisha utayari wa oparesheni, kuwapa kipaumbele maafisa wa idara hiyo na kuendeleza mikakati ya usalama wa taifa.

Jenerali Kahariri ametoa hakikisho hilo wakati wa ziara yake katika kambi ya jeshi la wanamaji ya Manda Bay kaunti ya Lamu, na vile vile amekutana na wanajeshi wa KDF wanaoendeleza oparesheni ya Amani Boni.

Kwenye maelezo yake wakati akihutubia maafisa hao Jenerali Kahariri amewapongeza wanajeshi hao akisema wameonyesha tajriba ya hali ya juu na kujitolea katika ulinzi wa taifa.

Mkuu huyo wa majeshi aidha amegusia mipango inayoendelezwa ya miradi ya kisasa jeshini, akisema wanalenga kuwekeza zaidi ili kuimarisha uwezo wa wanajeshi kufanikisha oparesheni za kiusalama.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.