Monday, 19January, 2026    8:03 am

Play Listen Live
IEBC

Mpiga Kura Awasilisha Kesi Akitaka Kusitishwa Maandalizi ya Uchaguzi wa 2027

Mpiga kura Benard Mwanzia amewasilisha kesi katika mahakama kuu, akiitaka mahakama kusitisha maandalizi yote ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, yanayoendelezwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC. Katika kesi hiyo Mwanzia ameibua maswali ya kikatiba kuhusu uhalali na uthabiti wa mfumo wa uchaguzi nchini, akiitaka mahakama kuidhinisha kesi hiyo kuwa ya dharura. Mwanzia katika kesi hiyo vile vile anaitaka mahakama kuzuia tume ya IEBC,mawakala na wafanyikazi wa tume hiyo dhidi ya kutumia rasilimali za umma kwa ajili ya maandili ya uchaguzi hadi pale kesi hiyo itakaamuliwa. Mwanzia amesema iwapo mahakama haitoingilia kati, IEBC itaendelea kutumia rasilimali za umma kuendeleza michakato ambayo baadaye itatajwa kuwa kinyume cha katiba.

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.