Mwamambi yawika katika mashindano ya kutoa huduma za kwanza

April 3, 2017

Na Dominick Mwambui

Kwale, KENYA, Aprili 4 – Shule ya msingi ya Mwamambi waliwika katika awamu ya kwanza ya mashindano ya kutoa huduma za kwanza katika kitengo cha shule za msingi yaliyofanyika wikendi.

Katika kitengo cha shule za upili, shule ya wasichana ya Kwale Girls ilichukua taji hilo huku  Dr. Babla School ikichukua nafasi ya pili.

Katika kitengo cha vyuo vya kiufundi, KMTC Msambweni ilinyakua ushindi na kufuatwa na KMTC Kwale.

Akizungumza wakati wa kuzawadi washindi, naibu mwenyekiti wa shirika la msalaba mwekundu tawi la kwale, Jida Bakara alisema mashindano hayo yanalenga kuimarisha ujuzi wa viwango vya kutoa huduma ya kwanza wakati wa mikasa.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.