Picha Kwa Hisani – The Standard
Story by: Taalia Kwekwe
Mahakama ya mjini Kwale imemuhukumu kifo mwanamume mmoja kwa Jina Joseph Olouch Odhiambo baada ya kupatikana na hatia ya kutekeleza wizi wa mabavu.
Kulingana na maelezo yaliotolewa mahakamani, mshatakiwa mnamo tarehe 6 mwezi Novemba mwaka 2018, alitekeleza wizi wa mabavu katika jumba la Villa La Spa,huko Diani, na kuiba bidhaa mbali mbali zenye thamani ya shilingi milioni moja elfu 41,500 mali ya Karl Salzmann aliye raia wa ujerumani.
Picha Kwa Hisani – The Guardian
Hakimu wa mahakama hio Joe Omido amesema ametoa uamuzi huo baada ya kuzingatia ushahidi wa kina uliowasilishwa mahakamani na kwamba mwanamume huyo atatumikia kifungo chake katika gereza la Migingo. kaunti ya Kwale.
Awali hakimu Omido alimuachilia huru mwanamume mmoja Daniel Oweret Ouko ambaye aliaminika kushirikiana na mshtakiwa huyo,hii ni baada ya kutompata na hatia., Odhiambo amepewa siku 14 za kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.