Naibu katibu mkuu wa chama cha UDA Daniel Ole Sambu, ameaga dunia siku ya Alhamisi.
Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar Sarai amesema Ole Sambu alikua nguzo katika chama cha UDA na alikua nguvu kuu ya kuimarisha chama hicho mashinani.
Sarai amesema Ole Sambu alikua na maono ya kimkakati, alijitolea kikamilifu kuimarisha chama hicho, akisema kifo cha kiongozi huyo ni pigo kwa chama na kwa familia yake.
Ole Sambu ameaga dunia ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kumkaribisha rais William Ruto katika tamasha la utamaduni na utalii la jamii ya Maa huko Amboseli.
Story by Mimuh Mohamed



