Tuesday, 16December, 2025    6:48 pm

Play Listen Live
ODm

ODM Yajizatiti Kuimarisha Umoja na Uthabiti Kabla ya Uchaguzi wa 2027

Chama cha ODM kinapaswa kuwa imara hata zaidi na kuendelea kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Seneta wa Kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo aliye Kiongozi wa wachache katika Bunge la Seneti amehoji kwamba kwa sasa jambo la msingi chamani ni kujenga udhabiti wa chama na kuziba mianya ya mgawanyiko na malumbano ili chama hicho kisiporomoke. Kulingana na Madzayo, si kinyume kwa chama hicho kuungana na vyama vingine vya kisiasa katika kuunda Serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027, akiwataka wanachama na Viongozi wa chama cha ODM kumakinika katika kukidhibiti chama. Kauli sawa na hiyo ilitolewa hapo awali na Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna aliyehoji kwamba umoja wa chama ndiyo kipengele kikuu atakachokitilia mkazo katika uongozi wake. Semi hizo zinajiri huku Kaunti ya Mombasa ikijiandaa kwa shamrashamra za kuadhimisha miaka 20, tangu kuasisiwa kwa chama hicho, sherehe zitakazoanza Novemba 14 hadi 16 mwaka huu.  

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.