Picha kwa Hisani –
Wafanyikazi wawili wa Mahakama ya Rufaa mjini Mombasa wamenusurika baada ya paa la jengo la Mahakama hiyo kuporomoka.
Wakizungumza na Wanahabari baada ya mkaso huo, wafanyikazi katika afisi za Msajili wa kesi katika Mahakama hiyo, wamesema tangu jengo hilo kurekebishwa upya limekuwa na matatizo mengi.
Wafanyikazi hao wamesisitiza umuhimu wa kuhamishwa katika afisi zengine, wakisema jengo hilo sio salama kwa maisha yao.
Hata hivyo shuhuli zote zinazoendelea katika Mahakama hiyo zimesitishwa kwa muda usiojulikana.