Monday, 19January, 2026    8:39 am

Play Listen Live

Rais Ruto analenga kuingia kwenye makubaliano mapya na chama cha ODM ya kuunda serikali ya pamoja mwaka 2027.

Kwa mara nyengine tena rais William Ruto ameeleza azma yake ya kuendelea kufanya kazi na chama cha ODM hadi wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027.

Akizungumza siku ya Jumatano katika kaunti ya Migori rais Ruto amefichua kwamba analenga kuingia kwenye makubaliano mapya na chama cha ODM ya kuunda serikali ya pamoja mwaka 2027.

Rais Ruto aidha amewataka viongozi wa chama hicho kuweka mikakati ya kuimarisha chama hicho, akisema mgawanyiko miongoni mwa wanachama wa ODM utasambaratisha chama hicho.

Kiongozi wa nchi  amesema iwapo viongozi wa ODM watafanya chama hicho kuwa na nguvu zaidi, chama cha UDA kitajipanga zaidi, ili vyama hivyo viwili viungane na kuunda serikali ijayo.

 

Story by  Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.