Rais wa chama cha wahasibu barani Afrika ACCA Melanie Proffitt amewataka wadau katika sekta hiyo kuzingatia uwajibikaji na uadilifu katika utendakazi wao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la wanachama wa chama hicho,Bi.Proffitt amesema iwapo wadau wa sekta hiyo watazingatia masuala hayo muhimu wataimarisha sekta hiyo bara Afrika.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa chama hicho kanda ya Afrika Mashariki George Njeri amesema chama hicho kinazingatia uadilifu sawa na kupambana ufisadi miongoni mwa wanachama wao.
Naye mkuu wa masuala ya umma katika chama hicho Bi.Jane Ohadike amesema chama hicho kinalenga kushirikiana na wadau wengine ili kuimarisha taaluma ya uhasibu.
Story by Bakari Ali



