Tuesday, 16December, 2025    6:32 pm

Play Listen Live

Rwanda Air imerudisha rasmi safari za ndege kutoka taifa la Rwanda hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi jijini Mombasa.

Sekta ya utalii nchini imepigwa jeki baada ya kampuni ya usafiri wa angani ya Rwanda Air kurudisha rasmi safari za ndege kutoka taifa la Rwanda hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi jijini Mombasa.

Kupitia kwa barua rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na viwanda nchini KNCCI tawi la Mombasa Abud Jamal amepongeza hatua ya usimamizi wa kampuni hiyo kurudisha safari hizo baada ya kukatizwa kwa takriban miaka 5.

Abud vilevile amepongeza serikali ya kaunti ya Mombasa na ile ya kitaifa kufungua angavu kwa kampuni mbalimbali za kimataifa kuweza kutumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi hali itakayoimarisha uchumi wa kaunti ya Mombasa,Pwani na taifa kwa jumla.

Haya yanajiri siku chache baada ya kampuni ya usafiri wa angani ya Turkish Airline kuanzisha safari za kutoka uturuki hadi uwanja huo na kuongeza idadi ya ndege za kimatifa kutumia uwanja huo huku ikiwa ni mda baada ya seneta maalum Bi.Miraj Abdillahi kuishinikiza serikali kupitia kwa wizara ya uchukuzu na ile ya utalii kuzingatia sheria ya Open Sky policies ili kuruhusu ndege za kimataifa kutumia uwanja huo na kukuza utalii na uchumi wa kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla.

Story by Bakari Ali Bakari

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.