Monday, 19January, 2026    7:58 am

Play Listen Live

Sekta ya afya nchini huenda ikasambaratika baada ya matabibu kutoa notisi ya mgomo.

Muungano wa matabibu nchini ‘Kenya Union of Clinical Officers’ umetoa notisi ya siku 21 ya kushiriki mgomo, ukilaumu wizara ya afya na baraza la magavana nchini kwa kutotimiza makubaliano muhimu ya Leba.

Katibu mkuu wa muungano huo George Gibore amesema serikali imeshindwa kutimiza mkataba wa kurejea kazini uliotiwa saini mnamo Julai 8, mwaka huu 2025, na mkataba mwengine uliotiwa saini kati ya matabibu na wizara ya afya mnamo  Julai 27, Mwaka 2024.

Katika barua aliyoituma kwa wizara ya afya na baraza la magavana,  Gibore amesema makubaliano hayo yalilenga kutoa nafasi ya kutiwa saini, kusajiliwa na kutekelezwa mkataba wa makubaliano ya malipo CBA.

Gibore amesema kuchelewa kuukamilisha mkataba huo wa malipo, kumepelekea wahudumu wa afya kuendelea kufanya kazi katika mazingira yasiyo salama, baadhi wakipata matatizo ya afya ya akili kutokana na malipo duni na changamoto nyengine za kikazi.

Gibore ameizilaumu baadhi ya serikali za kaunti kwa misingi kwamba zimekiuka wazi wazi muongozo mpya wa malipo uliotolewa na tume ya kutahmini mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa umma SRC

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.