Story by Charo Banda –
Waziri wa maji na unyunyizaji mimea Bi Sicily Kariuki amesema serikali ina mipango ya kufufua upya mradi wa Galana Kulalu ili kuhakikisha unazalisha chakula kwa wingi.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuzuru katika mradi huo, Sicily amesema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mradi huo wa kilimo nyunyizi wa takriban ekari elfu 540 unaongezwa hadi ekari milioni moja.
Sicily amesema mpango wa unyunyizaji maji mashamba utasaidia pakubwa mradi huo kuzalisha chakula kwa wingi ili kukabiliana na ukame na baa la njaa linaloendelea kushuhudiwa nchini.
Wakati uo huo amedokeza kuwa serikali ina mipango ya kuhakikisha mradi huo unakabidhiwa muekezaji wa kibinafsi ili kufanikisha malengo ya serikali ya kuzalisha chakula.