Mwakilishi wa baraza la watu wanaoishi na ulemavu Emily Mwembe ameeleza haja ya kuzingatiwa kikamilifu haki za watu wenye uwezo maalum.
Akizungumza wakati maadhimisho ya siku ya watu wenye mahitaji maalum, katika shule ya wenye mahitaji maalum ya Kinango Mwembe amehimiza ikiwemo kuweka watafsiri wa lugha ya isha katika ofisi za umma.
Naye gavana wa kaunti ya Kwale Bi Fatuma Achani amewataka wakaazi kuwasajili watoto wenye mahitaji maalum ili wanufaike na miradi ya serikali inayowalenga, huku naibu gavana Chirema Kombo akiwasihi wazazi wenye uwezo maalum kutowaficha watoto hao.
Story by Kombo Mangale



