Story by Ephie Harusi –
Serikali ya kaunti ya Kilifi kupitia idara ya michezo imeahidi kuwekeza katika sekta ya michezo ili kuinua vipaji vya vijana katika kaunti hiyo.
Katibu wa michezo katika Wizara ya fedha kaunti ya Kilifi, Ben Kai amesema tayari mikakati ya kuboresha viwanja vya kaunti hiyo na muundo msingi inaendelea ili kuwawezesha vijana kuwa na viwanja vya kisasa.
Akizungumza katika eneo la Tezo baada ya kushuhudia mechi ya Jumhuri Cup, Kai amesema mikakati hiyo itachangia vijana wenye vipaji mbalimbali kutambulika na kujiimarisha kimaisha kupitia talanta zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jamhuri Cup Israel Yeri, amesema japo baadhi ya vijana katika kaunti hiyo wamekosa kuboresha vipaji vyao kutokana na changamoto za viwanja ni lazima serikali ya kaunti ya Kilifi ilifikia swala hilo ili kukuza vipaji vya vijana kupitia Soka.