Serikali yahimizwa kutilia manani Karate

April 7, 2017

Na: Charo Banda

Malindi,  KENYA, Aprili 7 – Mwenyekiti wa Kenya Karate Technical Commisions  Anderson Shillingi ameirai serikali kuhakikisha kuwa mchezo wa Karate unatiliwa maanani kama michezo mingine  ili kuwapa uwezo vijana kuweza kukuza talanta zao kupitia mchezo huo.

Shilingi amesema kuwa endapo serikali itaipa uwezo zaidi timu za mchezo huo basi vijana wengi ambao wamekosa ajira na kujiingiza kwenye utumizi wa mihadarati wataokolewa.

Shilingi ameongeza kuwa kuna zaidi ya timu 30 zitakazoshiriki  mashindano ya world karate championship yatakayofanyika huko Watamu  katika ukumbi wa Watamu Sports and Leisure academy.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.