Monday, 19January, 2026    8:53 am

Play Listen Live

Stanley Kenga wa chama cha DCP atangaza azma ya kuwania tena nafasi ya ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Siku chache tu baada Stanley Kenga wa chama cha DCP kushindwa kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge wa Magarini kaunti ya Kilifi, kiongozi huyo sasa ametangaza azma ya kuwania tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Akizungumza katika eneo la Magarini Kenga amesema kwa sasa anaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha anapata uungwaji mkono katika uchaguzi ujao.

Kauli yake imeungwa mkono na baadhi ya wafuasi wake, waliodai kwamba Kenga alishindwa kwenye uchaguzi mdogo wa Magarini, baada ya mpinzani wake wa karibu kuwapa hongo wapiga kura.

Katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Magarini ulioandaliwa Novemba 27, Kenga aliibuka wa pili baada ya kupata kura elfu 8,907, huku mpinzani wake Harrison Kombe wa ODM aKichukua ushindi kwa kupata kura 17,909

 

Story by Manlex Ngombo

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.