Mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la Kaunti ya Mombasa Kibwana Swaleh Baya amesema kuwa ni sharti walanguzi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Mombasa na kwengineko Pwani kuadhibiwa vikali ili kukabiliana vilivyo na ulanguzi.
Swaleh amependekeza washukiwa wa ulanguzi wanaofikishwa mahakamani kutozwa dhamana za juu badala ya kuwekewa dhamana wanazoweza kumudu kwa urahisi.
Akizungumza Mjini Mombasa, Mwenyekiti huyo wa kamati ya afya katika bunge la Kaunti ya Mombasa amesema kwamba mara nyingi walanguzi wamelipia dhamana wanazotozwa na kuendeleza biashara hiyo haramu.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni