Monday, 19January, 2026    7:30 am

Play Listen Live

UDA kumuidhinisha Jimmy Kahindi kuwa mgombea wake wa ugavana kaunti ya Kilifi.

Chama cha UDA kimeweka wazi kwamba kitamuidhinisha aliyekua spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi, kuwa mgombea wake wa ugavana wa kaunti ya Kilifi katika uchaguzi ujao.

Chama cha UDA kimeafikia uamuzi huo, baada aliyekua waziri wa jinsia nchini Aisha Jumwa kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha PAA kinachoongozwa na spika wa bunge la seneti Amason Jeffa Kingi.

Akizungumza katika kanisa la ACK Holy Trinity huko Kericho, katibu mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar Sarai, amesema chama cha UDA kitaidhinisha wagombea katika maeneo yote wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kufuatia tangazo hilo la chama cha UDA, kipute cha ugavana kaunti ya Kilifi katika uchaguzi mkuu ujao huenda kikashuhudia ushindani mkali kati gavana wa sasa Gideon Mung’aro, Aisha Jumwa, Jimmy Kahindi na wakili George Kithi miongoni mwa wengine.

Chama chama UDA kinaendeleza mikakati ya kujiimarisha zaidi mashinani, uchaguzi wa mashinani wa chama hicho ukiratibiwa kufanyika Januria 10, Mwaka 2026.

 

Story by Mimuh Mohamed

 

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.