Kenya imeungana na mataifa mengine ulimwenguni siku ya Jumatano tarehe 3 ya mwezi Disemba, katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye uatilifu.
Shirika la afya duniani WHO kwenye ripoti yake limesema linaangazia zaidi, jinsi ufadhili wa kifedha jumuishi unaweza kuleta mabadiliko katika maisha, afya na maslahi ya watu wanaoishi na ulemavu.
WHO imesema kote duniani watu bilioni 1.3 wanaishi na ulemavu i, na kwamba ili kufanikisha azma ya afya kwa wote, lazima mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum yaangaziwe kikamilifu.
Shirika hilo la afya duniani limesema huduma za afya zitasalia kutofikiwa, iwapo mifumo ya ufadhili wa afya itashindwa kuangazia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi wa shirika la WHO barani Afrika Dkt Mohamed Janabi amesema katika bara la afrika zaidi ya watu milioni 188 wanaishi na ulemavu.
Janabi ametaja magonjwa yakuambukiza na yasioambukiza, utapia mlo majeruhi na matokeo ya mizozo yote, kama kati ya mambo yanayochangia ulemavu, ingawa wanaishi na ulemavu wanatengwa, katika jamii, mara kwa mara wanapitia unyanyapaa, na vikwazo katika kupata huduma za afya, elimu, uchukuzi na ajira.



