Baadhi ya walimu wa shule za sekondari msingi katika kaunti ya Mombasa wameitaka wizara ya elimu nchini na wadau katika sekta hiyo kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na mtaala mpya wa elimu sawia na matokeo ya mitihani ya mitaala hiyo.
Akizungumza baada ya kupokea matokeo ya wanafunzi wa shule ya kijamii ya Bhadala Comprehensive katika kaunti ya Mombasa mwalimu mkuu wa shule hiyo Joyce Aswani amesema kuna haja ya jamii hususan wazazi kupata ufahamu kamili wa mtaala huo ili kuweza kuwelea na kusaidia katika kuwendeleza na kuimarisha hali ya kielimu ya wana wao.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliyofanya vyema katika shule hiyo wakiongozwa na Abdallah Madwani,Yahya Anwar na Sukeina Rashid wamepongeza ushirikiano kati ya walimu,wazazi na usimamizi wa shule hiyo kwa kuwasaidia kufanya vyema katika mitihani hiyo.
Naye mmoja wa wasimamizi wa shule hiyo Sajeed Ismael amepongeza ushirikiano wa wadau husika kwa kufanikisha maendeleo ya shule hiyo.



