Monday, 19January, 2026    8:08 am

Play Listen Live

Wafanyibiashara kutoka kaunti ya Kwale wamehimizwa kutumia fursa ya maonyesho ya biashara ya Diani Business &Trade Expo 2025 ili kutangaza biashara zao.

Wafanyibiashara kutoka kaunti ya Kwale wamehimizwa kutumia fursa ya maonyesho ya biashara ya Diani Business &Trade Expo 2025 ili kutangaza biashara zao.

Akizungumza baada ufunguzi wa maonyesho hayo katika eneo la Ukunda mwenyekiti wa kamati wa kamati ya bunge la kaunti ya Kwale kuhusu biashara ambae pia ni mwakilishi wa wadi Tiwi  Juma Mwachivyomo amesema bunge hilo litaidhinisha sera ya kutoa mikpo ya riba ya chini ya wafanyibiashara.

Kwa upande wake mkurugenzi wa biashara katika  serikali ya kaunti ya Kwale  Heidi Mumia, amewataka wafanyabiashara kutumia  maonyesho hayo kubadilishana mawazo ya kibiashara.

Maonyesho hayo ya siku tatu yanalenga kuunganisha wafanyabiashara na wateja sawa kuhakikisha wanapata soko zaidi la biashara zao.

 

Story by Rasi Mangale

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.