Monday, 19January, 2026    8:50 am

Play Listen Live

Wakenya kusherehekea sherehe za 62 za siku ya Jamhuri Disemba 12.

Wizara ya usalama wa ndani imetangaza mkakati wa kiusalama kabla ya sherehe za maadhimisho ya 62 ya siku ya Jamhuri zitakazofanyika kesho Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Mshirikishi wa utawala Gilbert Kitiyo amewataka wakenya wanaopanga kuhudhuria sherehe hizo, kuwa waangalifu na kuzingatia maagizo ya kiusalama yanayotolewa na mamlaka husika.

Kitiyo amesema sherehe za mwaka huu zinatarajiwa kuvutia idadi kubwa ya watu ikiwemo maafisa wakuu serikalini na viongozi wa kigeni, hatua ambayo inalazimu kuongeza idadi ya maafisa wa usalama kudhibiti usalama.

Kitiyo aidha amewataka wananchi kuwa makini wanapokua kwenye mikusanyiko, kwani wahalifu hutumia fursa hiyo kuwaibia wananchi vitu vya thamani ikiwemo Simu.

Wizara ya usalama wa ndani imesema itatuma timu ya vitengo tofauti vya usalama ikiongozwa na idara ya polisi na maafisa wa huduma ya vijana kwa taifa NYS.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.