Story by Gabriel Mwaganjoni –
Jaji mkuu nchini Martha Koome hapaswi kukashfiwa kwani ana tajriba inayostahili katika kutekeleza majukumu yote ya afisi ya Jaji mkuu nchini.
Ni kauli iliyotolewa na Wakili Jane Kimori aliyesema Jaji Koome ni Jaji aliyehudumu katika idara ya mahakama kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 na juhudi zake zimechangia mabadiliko makubwa kwenye idara ya mahakama.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Wakili Kimori amesema ni vyema iwapo Jaji Koome atapewe muda katika kupigania haki za wakenya na wala sio kukosolewa na kudhalilishwa bila ya sababu zozote msingi.
Kulingana na Wakili huyo Jaji Koome anachukua wadhfa huo wakati tayari Jaji mkuu mstaafu David Maraga alikuwa ameiweka idara ya mahakama kileleni katika kupigania usawa na haki na kazi hiyo ndio Koome anapaswa kuifanya.