Wakulima katika kaunti ya Taita taveta wameonywa dhidi ya kununua dawa za kuua wadudu kwa wachuuzi na maduka ambayo hayajaidhinishwa, wakati huu ambapo kunashuhudiwa ongezeko la uuzaji bidhaa gushi na zisizosalama.
Haya yamesemwa na waziri wa kilimo katika serikali ya kaunti hiyo Dawson Katuu Mzenge, wakati serikali ya kaunti hiyo ikiendeleza kampeni ya kuhakikisha kilimo salama ndani ya kaunti hiyo.
Katuu amewataka wakulima katika kaunti hiyo kuzingatia muongozo wa utumizi salama wa dawa za kuua wadudu, ili kupunguza kutegemea chemikali hatari.
Bodi ya kudhibiti dawa za kuua wadudu Pest Control products Board, imeonya kwamba dawa za kuua wadudu zinazouzwa kiholela na zinazoingizwa nchini kimagendo kutoka Tanzania,hazijaidhinishwa na zinahatarisha afya ya binadamu
Story by Mimuh Mohamed



