Mgombea wa nafasi ya naibu mwenyekiti wa chama wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET tawi la kaunti ya Kwale Hamza Abdalla Musa, amewahimiza walimu kuchagua viongozi watakaosimama kidete kutetea maslahi yao, katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Januari 2026.
Akizungumza baada ya kuwasilisha stakabadhi zake katika afisi za KUPPET mjini Kwale mapema leo, Hamza ambaye anawania nafasi hiyo kwa muhula wa pili amesema ana uzoefu utakaomuwezesha kulinda masalahi ya walimu.
Kwa upande wake katibu wa chama cha KUPPET kaunti ya Kwale Leonard Oronje amesema walimu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiweko bima ya afya na uhaba wa walimu katika baadhi ya shule.
Oronje amesema chama cha KUPPET kitahakikisha serikali kupitia tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC inawapa walimu wa shule za sekondari msingi mikataba ya kudumu.
Story by Rasi Mangale



