Maafisa wa polisi katika eneo la Diani kaunti ya Kwale wamewatia nguvuni watu watatu wanaoshukiwa kuendeleza biashara haramu ya kusambaza pesa bandia katika kaunti ya Mombasa na maeneo jirani.
Kulingana na ripoti ya idara ya upelelezi wa jinai DCI, watatu hao Fadhili Lawrence, Atemba Lawrence na Electrine Okwako, wametiwa nguvuni wakiwa mafichoni huko Diani ambako wanaendeleza biashara hiyo.
Maafisa wa DCI wameripoti kwamba watatu hao wamepatwa na pesa bandia shilingi milioni 1.7, zikiwa katika sarafu ya shilingi elfu moja zikiwa zimefichwa kwenye bagi la kipakatalishi au Laptop.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba watatu hao ni kati ya mtandao wa wahalifu wanaosambasa pesa bandia katika maeneo tofauti ya ukanda wa Pwani.



