Wetangula kuunga mkono mgombea yoyote wa NASA

April 10, 2017

Na: Michael Otieno

Kinara wa Chama cha Ford Kenya, Moses Wetangula amesema kuwa ataunga mkono yeyote miongoni mwao, atakaeteuliwa kugombea wadhfa wa Urais kwa tiketi ya Muungano wa NASA.

Wetangula ameilaumu serikali ya Jubilee kwa kuendeleza dhulma dhidi ya wakaazi wa Pwani huku akikiri kuwa chama cha Ford Kenya, kitamuunga mkono Balozi Chirau Ali Mwakwere kuwania kiti cha Ugavana kaunti ya Kwale.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.