Monday, 19January, 2026    8:42 am

Play Listen Live

Zaidi ya vijana 80 wadi ya Mjambere wanufaika na masomo ya kiufundi.

Zaidi ya vijana 80 kutoka wadi ya Mjambere gatuzi dogo la Kisauni wamenufaika na masomo ya kusuka, urembo,vipodozi na mapambo kutoka kwa wakfu wa Amriyah Juma Boy kama njia moja wapo ya kujiendeleza kiujuzi na kimaisha.

Akizungumza kwenye hafla ya kufuzu kwa wanafunzi hao mdhamini mkuu wa masomo hayo wakili Amriyah Boy ambaye pia ni mwakilishi wadi wa eneo hilo amesema masomo hayo yanalenga kusaidia vijana hao kimaisha sawia na kuwaepusha na masuala potofu kwa jamii.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswammad Sharrif Nassir amewarai wawakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Mombasa kupitisha mswada maalum wa fedha za maendeleo ya wanawake na vijana katika kaunti hiyo ili kuweza kusaidia kuimarisha miradi kama hiyo katika kaunti ya Mombasa.

Naye mbunge wa Kisauni Rashid Juma Bedzimba amesisitiza ushirikiano wake na vijana hao katika kuwaendeleza kimaisha.

Story by Bakari Ali Bakari

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.