Tuesday, 16December, 2025    6:54 pm

Play Listen Live

Zamzam Mohamed Akanusha Madai ya Ufujaji wa Fedha za NGAAF Mombasa

Mwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa Bi Zam zam Mohamed, amekanusha madai kwamba ofisi yake imejihusisha na ufujaji wa fedha za hazina ya NGAAF. Katika mahojiano na mwanahabari wetu, Zam zam amesema makundi yaliokosa fedha za hazina hiyo katika awamu ya kwanza ya ugavi wa fedha hizo, zimepata fursa katika awamu ya pili ya ugavi huo. Zamzam amekosoa hatua ya baadhi ya watu kueneza propaganda kuhusiana na ugavi wa fedha hizo, akisema watu hao hawana ufahamu kuhusu usimamizi wa hazina hiyo. Zam zam aidha amesema hatashurutishwa na wapinzani wake wa kisiasa katika kutekeleza majukumu yake kwa wakaazi wa kaunti hiyo.  

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.