Monday, 19January, 2026    9:08 am

Play Listen Live

Zoezi la kuchagulia shule wanafunzi wa gredi ya 10 kuanza katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Waziri wa elimu nchini Julius Ogamba amesema zoezi la kuchagulia shule wanafunzi wa gredi ya 10 litafanyika ndani ya wiki mbili zijazo na wanafunzi hao wanatarajiwa kuripoti katika shule watakazosomea tarehe 12 mwezi ujao wa Januari.

Akizungumza jijini Nairobi wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani wa KJSEA kwa wanafunzi wa gredi ya 9, Ogamba amesema wanafunzi wote kwa sasa wanaweza kupata matokeo yao.

Kulingana na Ogamba kati ya watahiniwa milioni 1, elfu 130,459 waliofanya mtihani wa KJSEA, asilimia 59.09 wameonyesha uwezo wa kufanya masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu maarufu STEM wanapoingia shule za sekondari ya juu, pamoja na masomo ya sayansi jamii, sanaa na sayansi michezo.

Ogamba aidha ameongeza kwamba asilimia 46.25 ya watahiniwa hao wameonyesha uwezo wa kufanya sayansi jamii, huku asilimia 48.73 kati yao wakionyesha uwezo wa kufanya masomo ya Sanaa na sayansi michezo.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.