Ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu kuanza mwezi Januari mwakani
Rais William Ruto ametangaza kwamba ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu utaanza rasmi mwezi Januari mwakani.
Katika hotuba yake rais Ruto amesema mradi wa barabara hiyo itakayoelekea hadi Malaba, ni mradi wa maendeleo uliopiganiwa na aliyekua waziri mkuu hayati Raila Odinga.
Rais Ruto amesema mradi huo wa reli ya kisasa kutoka Naivasha, Kisumu,hadi Malaba ulikua kwenye ajenda ya miundo msingi ya hayati Odinga.
Serikali pamoja na sekta ya reli wanakadiria kwamba mradi huo wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha-Kisumu- Malaba, utagharimu kati ya shilingi bilioni 646 hadi shilingi bilioni 648.
Reported By: Mimuh Mohamed